NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
UONGOZI wa Kanisa la Evangelist Assambless of God (EAGT) Jimbo la Dodoma Kusini limesema kuwa linawahimiza waumini wake kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kujiongezea kipato badala ya kutegemea miujiza.Anaripoti Danson Kaijage ,Dodoma(Endelea)
Hayo yameelezwa na askofu wa jimbo hilo,Barnaba Chilingo wakati wa ziara ya kuwatembelea viongozi wa kada mbalimbali katika kanisa hilo pamoja na kutoa semina ya uongozi.
Semina hizo zimekuwa zikiambatana na kutoa mwelekeo wa malengo ya kanisa hilo kwa muda wa miaka 15 hijayo ambayo yanalenga kuigusa jamii kwa kuwakomboa kimwili na Kiroho.
Akizungumzia mpango mkakati wa kanisa hilo Askofu Chilingo amesema kuwa kanisa limeweza kujenga ofisi ya makao makuu iliyopo Ilazo Jijini Dodoma.
Pia ameeleza kuwa uongozi wa kanisa hilo kwa kutekeleza mpango mkakati limeweza kujenga chuo kikuu cha Theologia kilichopo Jijini Dodoma chene ghorofa mbili,kuanzisha kituo cha Televisheni pamoja na kituo cha radio,aidha kanisa limeweza kununua shule ya sekondari iliyopo katika Mkoa Kahama.
Kutokana na mikakati hiyo ambayo inalenga zaidi kuinufaisha jamii kupitia katika uongozi wa kanisa hilo bado wanawahimiza waumini kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa ufanyaji wa kazi ni mpango wa Mungu mwenyewe.
Askofu huyo wa Jimbo la Dodoma,Kusini ameeleza kuwa ni wajibu wa kila muhumini kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuwezesha maendeleo ya kufikia malengo ya kanisa ,Taifa na mtu binafsi kwa kujiongezea kipato.
Kwa upande wa Makamu wa Askofu wa Kanisa la EAGT Dodoma Kusini,Patson Yhao,amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi Serikali ihakikishe inasimamia haki na kuwalinda wapiga kura na wanaochagaguliwa.
Hata hivyo amesema kuwa kanisa linaendelea kufanya maombi kwa ajili ya kulifanya taifa kuwa na amani na utulivu na kuhakikisha kila mmoja anafurahia rasilimali za taifa.
Kuhusu vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea amesema kuwa Serikali inatakiwa kutoa uwanja mpana kwa viongozi wa dini ili kutoa elimu kuanzia ngazi ya shule za msingi,Sekondari,Vyuo vikuu pamoja na kwenye miadhara kwa lengo la kuwajenga watoto na vijana kuwa na hofu ya kimungu.
Mwisho.