NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
MKUU wa Kitengo cha Kuthibiti Taka Ngumu katika jiji la Dodoma Dickson Kimaro ameagiza Watendaji wa Kata kuhakikisha wanafanya msako wa kuwakamata watu ambao hawajitokezi katika kufanya usafi kwenye maeneo yao.
Ametoa agizo hilo wakati wa kuhitimisha zoezi la usafi katika mtaa wa Mwaja Kata ya Chamwino jijini Dodoma uifanyika siku ya Jumamosi ya mwisho ya mwezi wa saba mwaka huu.
Kimaro amesema kuwa jukumu la usafi ni la mtu binafsi na kila raia anatakiwa kutambua kuwa usafi ni lazima kutekelezwa na kwa kushirikiana na wenzake pale inapobidi.
Kiongozi huyo amesema kutokana na kuwepo kwa watu wanaokaidi kushiriki katika zoezi la usafi ni wajibu wa Watendaji wa Mitaa kuwachukulia hatua za kuwakamata na kuwatoza faini kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Halmashauri.
“Kuna watu ambao wao kazi yao nikujifungia katika mageti na hawashiriki katika zoezi a kufanya usafi sasa na kuna baadhi ya akina Mama Lishe na baadhi ya watu wanaendesha Karakana za kutengeneza magari na nyenzo mbalimbali za usafiri.
“Watu hao wanazalisha taka akini cha ajabu inapofikia hatua ya kushiriki kujitokeza wao wanafunga mageti au miango yao na kuwaacha wenzao waendelee kusumbuka na uchafu kwa kufanya hivyo nawaagiza watendaji wa mitaa kùhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria”ameagiza Kimaro.
Lucas Evance Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino amewahamasisha wananchi wenye umri wa kupiga kura wajitokeze kwa kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura kura.
Pia amesema watu wote wenye sifa ya kupiga kura na tayari kadi zao zilipotea au kuharibika wanatakiwa kufika katika vituo vya kujiandikisha ili kurekebisha taarifa zao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chamwino jijini Dodoma,Jumanne Ngede ameendelea kuwahamasisha wananchi wake kuhakikisha wanajumuika katika shughuli za maendeleo