NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel money Timiza Akiba kwa ushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania wamezindua promosheni ya kuweka akiba kidijitali – itakayojulikana kama ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ .
Kupitia Promosheni hiyo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia Bajaji, Pikipiki Runinga ya flati pamoja na pesa tasilimu kila wanapoweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba
Airtel Money Timiza Akiba ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Money kuweka akiba kidijitail wakiwa popote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 28, 2023 wakati akitangaza kuzindua promosheni hiyo mpya, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema, ‘Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali.
” Airtel Money tunajisikia Fahari sana tunapoendeleza ubunifu katika huduma hii ya Airtel Money inayokuwa kwa kasi huku wateja wakijihudumia kidigitali kupitia Airtel Money, alisema Singano na kuongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na Benki ya Letshego Tanzania kuendesha promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili (wiki 8) kuanzia leo”
Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde itawazadia wateja wote wa Airtel Money wanaoweka akiba kupitia Timiza akiba kuanzia wiki hii ambapo hadi kufikia mwisho wa promoshen wateja 203 watakuwa wameibuka washindi wa promosheni hii.
Amebainisha kuwa” tutakuwa na droo moja kila wiki ambapo Wateja 25 watashijishindia sh.20,000 kila mmoja na tutawawekewa pesa zao za zawadi moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money, vilevile tutatoa zawadi ya bajaji mpya, pikipipiki mpya, pamoja na Runinga mpya (flatscreen) kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii.
Mmbando ameongeza’, “mteja yeyote wa Airtel Money mwenye Timiza akiba ambaye anawekeza kuanzia shilingi 20,000 kwa wiki anastahili kuingia kwenye shindano na anaweza kushinda mara moja tu wakati wa droo ya wiki. Pia ninawakaribisha wateja wa Airtel Money ambao hawajawahi kutumia huduma ya Timiza Akiba kuanza kutumia sasa na kupata nafasi ya kujishindia zawadi hizi kabambe kila wiki.
“Wateja hawahitaji kujiandikisha au kulipa ili kuingia kwenye droo, utatakiwa tu kuweka akiba kwenye Airtel Money Timiza akiba kisha moja kwa moja utapata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia”. alisema Mmbando
Naye Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Leah Phil amesema “Benki ya Letshego Tanzania tunajivunia ushirikiano wetu na Airtel Money kupitia huduma hii ya kujiwekezea kidijitali, tunawahakikishia watejawote wa Airtel Money wenaotumia Timiza Akiba kwamba watapata zawadi zao za ushindi kwenye akaunti zao za Airtel Money zao mara tu watakapotangazwa kuwa washindi”.
Ameeleza “Kuwekeza akiba ni rahisi Piga *150*60# chagua namba 6 kisha namba 1 na ubonyeze 3 uanze kuweka akiba kidijitali huku ukiwa umejiweka kwenye nafasi ya watakaoshinda Bajaji kwa mshindi wa Kwanza, Pikipiki kwa mshindi wa pili, Televisheni ya Kisasa kwa mshindi wa tatu au pesa taslimu za kila wiki.
Phil ameongeza kuwa “wateja watakaowekeza kupitia Timiza akiba pia watafaidika na riba ya hadi asilimia 4.5 kwa mwaka kwa kile kiwango watakuwa wamejiwekea ndani ya mwaka.