KAMPALA, UGANDA
JESHI la Polisi mjini Kampala nchini Uganda wanamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Joy Biira kwa tuhuma za kumkata mumewe sehemu za siri jambo lililosababisha kifo cha mwanaume huyo.
Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga amesema mwanamke huyo mkazi wa Tarafa ya Makindye jijini Kampala anatuhumiwa kusababisha kifo cha Benson Baluku ambaye alikuwa akiishi naye kama mume
Kwa mujibu wa polisi, marehemu alirejea nyumbani Machi 26 akiwa amelewa na kuanza kupigana na mkewe ambaye kila mara alimtuhumu kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa.
Polisi wamesema mume alimshika mkewe shingoni na kuanza kumnyonga hali iliyomfanya mke atoe kisu na kumkata sehemu za siri.