NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Kampuni ya Mantra Tanzania Rosatom inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium kwa juhudi zao wanazozifanya kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
Akizungumza mkoani hapa mwishoni mwa wiki , alipotembelea banda la Maonesho la Kampuni ya Mantra Tanzania kabla ya uzinduzi wa wiki ya kumbukizi ya miaka 117 ya Mashujaa wa vita vya Majimaji kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mahenge mjini Songea Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Kampuni hiyo inapaswa kupongezwa kwa namna inavyoshirikiana na jamii kutatua changamoto zinazowakabili
Ameeleza kuwa Kampuni hiyo wakiwa wadau muhimu wa maendeleo wameshiriki maonyesho ya wiki ya kumbukizi ya miaka 117 ya Mashujaa wa vita ya Majimaji kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira migodini na shughuli za kijamii ambazo wamekuwa wakizifanya
Amesema kuwa licha ya kampuni hiyo kutoa misaada hiyo kwa kutambua nguvu za Wananchi lakini bado kampuni hiyo inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea maendeleo Wananchi wake ambapo hadi sasa miradi mbalimbali imefanyika na inaendelea kufanyika.
Akizungumza kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika kumbukizi hizo Meneja uhusiano wa Mantra Khadija Kawawa amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo kila mwaka ambapo wanatumia fursa hiyo kueleza kwa kina shughuli ambazo zinafanywa mgodini na katika jamii
Kawawa amesema kuwa imekuwa ikijikita kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ambayo inaizunguka kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira, elimu ya ujasiliamali na misaada mbalimbali katika sekta za afya, ujenzi wa miundombinu ya elimu, maji, na ofisi za Serikali na kufadhili miradi mbalimbali kwenye jamii ambazo zinauzunguka mgodi