NA MWANDISHI WETU,DODOMA
LEO Septemba Mosi,2026, Waziri wa Madini Anthony Mavunde (MB) amekutana na wakurugeni wa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited mjini Dodoma kujadili maendeleo ya mradi wa mto Mkuju unaojihusisha na uchimbaji wa madini ya urani wilayani Namtumbo,Ruvuma.
Akiongoza ujumbe huo Vladislav Shulga amesema kuwa kampuni ya Mantra Tanzania Limited ipo tayari kuendelea na ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kipekee Tanzania na Afrika mapema iwezekanavyo ndani mapema Oktoba 2026 mwaka huu baada ya kuzinduliwa mtambo mdogo wa uchakataji wa Urani mwaka jana 2025.
Akizungumza katika mkutano huo,Waziri wa Madini Mavunde ameitaka Kampuni ya Mantra kuhakikisha hatua za uendelezaji mradi zinaendelea kwa kasi kubwa na pia ameuhakikishia uongozi wa Mantra Tanzania kuwa wataendelea kupata msaada wa serikali katika kila hatua ili kuhakikisha mradi huu unasonga mbele na kuanza uzalishaji ifikapo 2029.







