NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI ya NMB imetunukiwa tuzo kama mkopeshaji bora wa kilimo kwa mwaka 2025
Tuzo hiyo ilipokelewa na Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Nsolo Mlozi kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa Aceli Africa, Freddy Bob-Jones (wapili kulia) katika hafla maalum ya utoaji Tuzo katika hoteli ya Delta jijini Dar es Salaam.
Upokeaji wa tuzo hiyo ulishuhudiwa na meneja wa Aceli Africa nchini Tanzania, Mwallu Mwachanga,mwakilishi wa Benki kuu ya Tanzania, Aminiel Frank mwakilishi wa jumuiya ya Mabenki tanzania, Tusekelege Mwaikasu.
Huu ni mfululizo wa benki ya NMB kupata tuzo ndani ya wiki moja ambapo juzi huko nchini Dubai ilipokea tuzo ya kuwa benki ya kwanza Afrika Mashariki kuwa na MasterCard maalum kwa Wateja wake.

