NAIBUWaziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko leo Januari 22,2024 ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.
Akiwa nchini, Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Pia atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Reli ya TAZARA na eneo la makaburi ya Wataalamu wa kichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA pamoja na Makumbusho ya Taifa.