WADAU na wananchi kote nchini wametakiwa kupanda miti kwenye maeneo wanayoishi na katika taasisi zao ili kuwezesha utunzaji mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantumu Mahiza wakati wa zoezi la upandaji miti liliofanyika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma leo Oktoba 03, 2023.
Mahiza amesema jamii inatakiwa kuhamasika katika utunzaji wa mazingira ikiwepo kupata hewa safi pamoja na mvua zakutosha kuzalisha chakula.
“Tumekuja hapa kupanda miti kwa lengo kuhihamasisha jamii suala la kutunza mazingira sio la Serikali au Kikundi cha watu fulani ni jukumu letu sote tujitoe tutunze mazingira yetu” alisema Maiza
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Green Eco Tanzania Stanley Shibuda amesema Shirika hilo linahamasisha upandaji wa miti kwa nchi nzima na kwasasa limeanza kwa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kupanda miti 1500 na mpaka sasa wamehamaisha kupanda miti 300.