NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili wa Hazina , kabla ya uteuzi huo Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus , Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wakati huo Rais amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, kabla ya uteuzi huo Abdallah alikuwa mkurugenzi wa GimcoAfrica Limited.
Abdallah anachukua nafasi ya Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.
Aidha Rais amemteua Mussa Mohamed Makame kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) , kabla ya uteuzi huo Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC na pia ni mshauri mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania.
Makame anachukua nafasi ya Dk James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi huu umeanza februari 24, 2023