NA MUNIR SHEMWETA, WANMM, MLELE
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda amesheherekea Siku Kuu ya Krisimasi akiwa katika jimbo lake la Kavuu lililopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Akiwa jimboni humo, Naibu Waziri Pinda alishiriki ibada ya Krisimasi katika Kanisa Katoliki Parokia Teule ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibaoni ambako alishiriki pia harambee ya ya ujenzi wa Nyumba za Mapadri wa Kanisa hilo na kuahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji. Ujenzi wa nyumba hizo utagharimu Sh.Milioni 75.
Ibada hiyo ya Krisimasi katika kanisa hilo ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Aidha. Naibu Waziri Pinda akiwa eneo la Kibaoni ambapo ndipo yalipo makazi yake wilayani Mlele mkoani Katavi alijumuika na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakiwemo viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mlele katika kusheherekea siku hiyo ya Noeli.
Naibu Waziri Pinda yuko jimboni kwake katika jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi pamoja na mambo mengine kujumuika na wapiga kura wake kutafakari utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo hilo.