Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba (kulia), akisalimiana na Kiongozi wa jopo la wataalam waliowasili nchini kufanya tathmini ya uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, John Walsh, Jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba , akizungumza na wataalam wa kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, John Walsh (kulia) na Aurelien Mali, Jijini Dodoma. Moody’s wameanza kazi ya kuifanyia Tanzania Credit Rating.Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kufanya Tathmini ya Uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) John Walsh (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Aurelien Mali na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango Japhet Justin. Kulia ni Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dk Yamungu Kayandabila, Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Sauda Msemo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, baada ya kukutana Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi ya tathmini hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mtaalam wa kufanya tathmini ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s Aurelien Mali, Jijini Dodoma. Katikati ni Kiongozi wa Timu hiyo John Walsh. Moody’s wapo nchini kuifanyia Tanzania Credit Rating.