NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hasaan anaendelea kupeleka furaha na neema kwa watumisi wa umma hapa nchini
Waziri Kikwete ameyasema hayo leo Mei 7,2026 katika Mkutano wa Maofisa Tawala na Rasilimali watu unaoendelea Ukumbi wa AICC jijini hapa.
Aidha Kikwete amewakumbusha
Maofisa hao kutekeleza wajibu wao na kuleta furaha kwa watumishi wa umma.
na watanzania kwa ujumla
“Nimeyaeleza haya kufuatia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha maslahi ya Watumishi wa umma nchini yanaboreka.
” Uamuzi wa hivi karibuni wa Serikali kupandisha madaraja watumishi 219,042 ni hatua ya kihistoria katika kuimarisha utumishi wa umma nchini Tanzania.” amesisitiza Kikwete
Pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa hatua ya upandishaji madaraja na ongezeko la mishahara ya Watumishi limepata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia.
“Pamoja na ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma (2025) asilimia 35.1 ongezeko la kima cha chini sekta binafsi (2025/26) asilimia 33.4 ambapo Sekta mbalimbali zinakwenda athiriwa na maboresho haya ikiwemo afya, elimu, kilimo, mawasiliano, usafirishaji, nishati, viwanda, biashara, hoteli, michezo, uvuvi, baharini, madini ,utamaduni n.k ” amefafanua Waziri huyo.
Wakati huo huo,Waziri Kikwete ameeleza kuwa matokeo haya kitakwimu zinaonesha kasi ya mageuzi ya kiutumishi chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imebeba uongozi wa kimkakati unaoweka mbele ustawi wa watumishi na ufanisi wa taasisi za umma.





