*Wabeba Lumbesa hatarini kuugua figo
*WMA YATOA tahadhari
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
IMEELEZWA kuwa adhabu ya Kisheria kwa yeyote atayebainika kufanya udanganyifu katika mizani faini yake ni Sh.100,000 hadi Sh.Milioni 20 kwa kosa moja iwapo mtenda kosa atakiri kosa.
Aidha kwa kosa hilo hilo faini ni Sh.300,000 hadi Sh.Milioni 50 iwapo kesi itapwlekwa mahakamani.
Hayo yameelezwa na Ofisa Utendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo( WMA) Alban Kihulla wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari leo Septemba 11,2024 jijini Dar es salaam kueleza mafanikio na changamoto za WMA tangu ilipoanzishwa Mei 13,2002.
“Ni kosa kisheria kwa mfanyabiashara kuchezea mizani kwani adhabu yake ni Sh.100,000 hadi 20,000,000 kwa kosa moja iwapo atakiri kosa
” Na iwapo kesi itakwenda mahakamani basi adhabu yake ni faini ya Sh.300,000 hadi Sh.50,000,000 hivyo basi niwasihi wafanyabiashara kuacha mwenendo huo mara moja “amesisitiza Kihulla
Amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao tayari wameshachukuliwa hatua kutokana na udanganyifu huo na bado Kampeni ya ukaguzi wa mizani unaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambao unakwenda sambamba na kuwaelimisha juu ya kutumia vipimo sahihi.
Akizungumzia changamoto kubwa ambayo WMA inaendelea kupambana nayo hivi sasa juu ya vipimo Kihulla anesema ni suala la lumbesa kwenye mazao mbalimbali ambapo amebainisha kuwa ujazo sahihi unaotakiwa ni kilogramu 105 na iwapo uzito huo utazidi basi ni kosa kisheria hivyo taasisi yake inaendelea kutoa elimu kwa wakulima hususani madhara ya kiafya yatokanayo na lumbesa hususani kwa wabebaji wa mizigo
“Lumbesa ni ufungashaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya kifungashio kwa uzito zaidi ya ule unaokubalika kisheria / ujazaji wa kifungashio na kuweka kilemba
” Mojawapo ya athari ni wabebaji wa magunia ya nazao yaliyozidi uzito ( lumbesa) kuwa hatarini kuugua magonjwa ya figo kwa kuwa wengi wao hulazimika kutumia vinywaji vya kuongeza nguvu ( energy drinks)hivyo basi baada ya muda fulani hupata magonjwa kama hayo hivyo nishauri waache mara moja”amesisitiza
Kihulla amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa Lumbesa inadhoofisha uchumi wa Taifa kwa kumpunja mkulima,Halmashauri kukusanya na mapato pungufu.
Athari zingine ni uharibifu wa miundombinu kama vile barabara na mabomba
Katika hatua nyingine Kihulla ameeleza mikakati ya WMA ambapo amesema inajipanga kuingia kwenye maeneo mapya ya uhakiki wa vipimo,Kuendelea kutoa elimu kuhusiana na matakwa ya Sheria ya Vipimo.
Mikakati mingine kwa mujibu wa Kihulla ni kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji kazi na kuendelea kujenga uwezo (Mafunzo na ununuzi wa vifaa).