Reading: TASAC YATOA TAARIFA KUZAMA KWA MELI YA UVUVI “MV LEGACY” SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kwa Umma kuhusu tukio lakuzama kwa boti ya uvuvi “MV LEGACY” yenye namba ya usajili DS/L1175 inayomilikiwana Yakoub Juma Khamis na yenye urefu wa mita 11 na upana wa mita 1.7 iliyopatiwa Cheti cha Usajili na Ubora na TASAC kufanya shughuli za uvuvi mnamo tarehe06/03/2024.Mnamo tarehe 10/03/2024 majira ya 10:01 alasiri, kituo chetu cha kuratibu shughuli zautafutaji na uokoaji (MRCC) kilipokea taarifa ya kuzama kwa boti ya uvuvi “MV LEGACY”iliyotokea majira ya saa 9:50 jioni karibu na fukwe ya Coco Beach, Msasani, Wilaya yaKinondoni mjini Dar es salaam ambayo ilikuwa na jumla ya Mabaharia tisa (09)ikijumuisha Wavuvi sita (06), Mhandisi Mitambo mmoja (01) na Manahodha wawili (02).Kituo cha MRCC kilifanya jukumu lake la kisheria la kuratibu shughuli ya uokoaji kwakutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi (Wanamaji) na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kufanyajuhudi za kufika eneo la tukio na kufanya zoezi la uokoaji. Watu wote tisa wamefanikiwakuokolewa na wanaendelea vizuri kiafya bila ya kuwa na changamoto yoyote.Boti hiyo ambayo ilikuwa katika majaribio ya kiufundi baada ya matengenezo ya mifumoya uvuaji samaki kwa kukokota (Trawling), ilianza majaribio majira ya saa 3:00 asubuhiikitokea maeneo ya Tandavamba, Kivukoni na kufanya majaribio ya kuvua samakiwakizunguka katika maeneo yenye maji mafupi karibu na eneo la daraja jipya laTanzanite (Upanga) hadi Coco Beach (Oysterbay). Ilipofika majira ya saa 9:50 Alasiriwakati nahodha anabadilisha uelekeo wa boti kuelekea upande wa kulia ndipo kambamoja ya upande wa kushoto ikakatika na kusababisha uzito kelemea kwenye kamba yaupande wa kulia na ndipo uzito ulipohama ghafla na kuilazimisha boti kunywa majiupande wa kulia kisha kuzama.TASAC inaendelea kutoa rai kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo majini kuzingatiaSheria na Kanuni za udhibiti usafiri majini na kuhakikisha muda wote wanavalia majaketiokozi ili kujiepusha na maafa yanayoweza kusababishwa na tukio la ajali.Imetolewa na;Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu,Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
TASAC YATOA TAARIFA KUZAMA KWA MELI YA UVUVI “MV LEGACY” SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kwa Umma kuhusu tukio lakuzama kwa boti ya uvuvi “MV LEGACY” yenye namba ya usajili DS/L1175 inayomilikiwana Yakoub Juma Khamis na yenye urefu wa mita 11 na upana wa mita 1.7 iliyopatiwa Cheti cha Usajili na Ubora na TASAC kufanya shughuli za uvuvi mnamo tarehe06/03/2024.Mnamo tarehe 10/03/2024 majira ya 10:01 alasiri, kituo chetu cha kuratibu shughuli zautafutaji na uokoaji (MRCC) kilipokea taarifa ya kuzama kwa boti ya uvuvi “MV LEGACY”iliyotokea majira ya saa 9:50 jioni karibu na fukwe ya Coco Beach, Msasani, Wilaya yaKinondoni mjini Dar es salaam ambayo ilikuwa na jumla ya Mabaharia tisa (09)ikijumuisha Wavuvi sita (06), Mhandisi Mitambo mmoja (01) na Manahodha wawili (02).Kituo cha MRCC kilifanya jukumu lake la kisheria la kuratibu shughuli ya uokoaji kwakutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi (Wanamaji) na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kufanyajuhudi za kufika eneo la tukio na kufanya zoezi la uokoaji. Watu wote tisa wamefanikiwakuokolewa na wanaendelea vizuri kiafya bila ya kuwa na changamoto yoyote.Boti hiyo ambayo ilikuwa katika majaribio ya kiufundi baada ya matengenezo ya mifumoya uvuaji samaki kwa kukokota (Trawling), ilianza majaribio majira ya saa 3:00 asubuhiikitokea maeneo ya Tandavamba, Kivukoni na kufanya majaribio ya kuvua samakiwakizunguka katika maeneo yenye maji mafupi karibu na eneo la daraja jipya laTanzanite (Upanga) hadi Coco Beach (Oysterbay). Ilipofika majira ya saa 9:50 Alasiriwakati nahodha anabadilisha uelekeo wa boti kuelekea upande wa kulia ndipo kambamoja ya upande wa kushoto ikakatika na kusababisha uzito kelemea kwenye kamba yaupande wa kulia na ndipo uzito ulipohama ghafla na kuilazimisha boti kunywa majiupande wa kulia kisha kuzama.TASAC inaendelea kutoa rai kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo majini kuzingatiaSheria na Kanuni za udhibiti usafiri majini na kuhakikisha muda wote wanavalia majaketiokozi ili kujiepusha na maafa yanayoweza kusababishwa na tukio la ajali.Imetolewa na;Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu,Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).