NA CATHERINE SUNGURA,DAR ES SALAAM
HATIMAYE Mawasiliano yaliyokatika kwa siku tatu katika barabara ya Madale -Mbopo hadi Bunju wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam yamerejea.
Mawasiliano hayo ya urefu wa Kilometa 16.5 yamerejea kutoka na juhudi zilizofanywa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini( Tarura ) na sasa eneo hilo limeanza kupitika.