NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amelitwisha bunge mzigo wa mkataba wa bandari kwa kusema chombo hicho kina mamlaka ya kuupitisha au kutoupitisha mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii wa kuendesha bandari za Tanzania baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai.
Mbossa ameyasema hayo leo Juni 8, 2023 wakati akifanya mahojiano na redio moja ya jijini Dar es Salaam akifafanua sintofahamu iliyotokea baada ya kuenea kwa taarifa za mkataba huo wa awali uliosainiwa Oktoba, 2022 baina ya serikali hizo mbili.
Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu maslahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.
Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”ameeleza Mbossa