KAMPALA, UGANDA
RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amekutwa na Virusi vya Korona 19 baada ya moja ya vipimo vitatu vilivyofanyiwa kubainika kuwa na virusi.
Rais Museveni, amesema alianza kujisikia vibaya wakati akitoa hotuba kwa taifa jana Jumatano kabla ya kuamua kwenda kufanya vipimo.
Katibu wa mkuu wa Wizara ya afya, Diana Atwine, alisema rais amepata dalili za mafua lakini yuko katika hali nzuri na ataendelea na majukumu yake.
Alisema Rais amepangiwa utaratibu mpya wa kuzuia maambukizi ya UVIKO19 wakati akitekeleza majukumu yake ya Urais.