NA MWANDISHI WETU, KILIMANJARO
MAHAKAMA ya Wilaya Siha mkoani Kilimanjaro imemuhukumu Yonana Youzo (19), mfanyakazi wa ndani mkazi wa Kijiji cha Wiri wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro kwenda jela miaka mitano kwa kosa la shambulio kuu la kingono kwa mtoto wa miaka mitatu
Mwendesha Mashtaka wa Sherikali, Kurwa Mungo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo Petro Elibahati amesema tukio hilo limetokea Machi 6 , mwaka huu majira ya saa tatu usiku katika kijiji hicho.
Mwendesha mashitaka huyu amesema siku ya tukio nyakati za usiku mtoto huyo alikuwa na mama yake mzazi na mfanyakazi wa ndani wakiwa nyumbani ndipo mama mzazi wa mtoto huyu alitoka nje.
Aliporudi alishangaa mtoto wake akiwa amevuliwa nguo na alipochukua nguo hizo na kuikagua na kuona mbegu za kiume na alipombana kijana huyo, alikiri kumuingilia kwenye mapaja ya mtoto huyo.
Mshtakiwa alishika miguu ya mtoto na kuibana kisha kuingiza uume wake hadi akamaliza haja yake.
Kutokana na unyama huo Mahakama imemhukumu kwende jela miaka mitano ili iwe fundisho.