NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka timu za Simba na Yanga ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa kuhakikisha zinaongeza kasi ya kufunga zaidi kwa maana fedha zipo za kutosha.
“Ni imani yangu kwamba ile kasi ya iliyopo miguu ya milioni 5 kwa kila bao itaendelea kuwepo hata zitakapoondoka na niwahakikishie wale waliokuwa wakinitania jana kwamba nampigia Msigwa, amwambie refa amalize mpira mimi fedha zimekwisha.
“Nataka niwahakikishie bado zipo,endeleeni kuweka mipira kwenye nyavu ili mjenge jina la nchi yetu, “alisema Rais Samia.