NA MWANDISHI WETU
KIKOSI cha timu ya soka ya JKT Queens, leo Machi 9, 2023 katika uwanja wa Meja Generali Isamuhyo inawakaribisha Mabingwa Watetezi wa Ligi ya Wanawake Tanzania Bara kwa ajili ya kutafuta alama tatu muhimu.
JKT Queens inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya Simba inayoongoza ikiwa na alama 22 kileleni.
Kwa sasa ligi hiyo imeingia katika mzunguko wa pili na jana mitanange miwili ilipigwa ambapo, Ceasia Queens waliigagadua Alliance Girls kwa mabao 4-3 huku Baobab Queens wakiipa kisago Amani Queens cha mabao 3-0.
Mtanange mwingine unaopigwa leo ni Mkwawa Queens watakapowakaribisha The Tiger Queens na Fountain Gate Princess wataoneshana kazi na Yanga Princess katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.