NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuthibitisha ubunifu wake kwa kuwa kampuni ya kwanza kati ya wote wanaotoa huduma za mawasiliano nchini kuzindua aina mpya ya laini ya simu ya mkononi inayoitwa eSIM (laini inayounganishwa moja kwa moja na simu) .
Laini hiyo ya kidijitali inamwezesha mteja kutumia laini hiyo kwa matumizi yale yale ya mwenye laini ya simu halisi.
Kwa kuzindua laini hii ya kidijitali ya eSIM, Airtel inakuwa Kampuni ya kwanza mkononi kuzindua laini ya kidijitali eSIM.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 16, 2023 wakati wa kutambulisha laini hiyo ya kidijitali ya eSIM, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema kuwa “Airtel siku zote imekuwa ikiwekeza kwenye bidhaa na huduma zenye ubunifu ambazo zinaendeana na maisha ya kila siku ya kidigitali, tunajisikia Fahari sana kuwa wakwanza sokoni kuzindua laini hii ya eSIM kuthibitisha dhamira yetu ya kuwa mtandao wa kigitali.
Amesema”Airtel eSIM inakuja na faida nyingi ikilinganisha na laini za kawaida zikiwemo haraka na rahisi kuunganishwa mtandaoni.
Ameeleza kuwa, Ukiwa na eSIM, mteja anaweza kutumia hadi laini tano hivyo kuepuka mzigo usio wa lazima wa kubeba zaidi ya simu moja.
Aidha Singano amefafanua kuwa, eSIM inaweza kuunganishwa na iWatch yako wakati ambapo unafanya mazoezi iwe marathon au GYM unaendelea kuwa umeunganishwa na mtandao.
” Laini ya eSIM ni salama Zaidi – kwa kuwa huwezi kupoteza laini hiyo bila kupoteza simu yako kwani wote tunafahamu laini za kawaida kuna muda huwa zinapotea, kuibiwa na kutumika kwenye utapeli” amefafanua Singano
Aidha amebainisha kuwa, eSIM ni rafiki wa Mazingira kwa kuwa hakuna vile viambata vya plastiki wala vibati vinavyotolewa ukiwa unanunua laini yako ya eSIM.
Ameeainisha kiwa, Ikiwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara nje ya nchi eSIM itakuwa ni rahisi kwako kubadilisha mtandao ukiwa popote.
Singano amesema kuwa kwa sasa eSIM inapatikana nchini kwenye mtandao wa Airtel pekee na mteja anayetaka kubadilisha laini yake ya kawaida kuwa ya eSIM atembelee duka lolote la Airtel nchini ili kupata QR Code maalum itakayomwezesha kubadili laini yake kuwa eSIM papo hapo.
“Angalizo ni kwamba sio simu zote zina uwezo wa kutumia eSIM. Baadhi ya Simu zinakubali Matumizi ya eSIM ni Pamoja na, IPHONE , SAMSUNG, GOOGLE PIXEL na MOTOROLA Piga *#06# kuhakiki uwezo wa SIMU yako kisha angalia EID. alisema Singano huku akisisitiza kuwa faida kubwa ya kuwa na eSIM suala la usalama, kwamba huwezi kupoteza laini hiyo bila kupoteza simu yako kuna ugumu wa mtu kucheza na taarifa ukiwa eSIM”.ameeleza Singano
Airtel itaendelea kutambulisha bidhaa na huduma mpya za kusisimua kwa wateja wake huku tukihakikisha huduma bora na nafuu kwa wakati wote. Matarajio na mahitaji ya wateja wetu yanabadilika na Airtel tuna uhakika kwamba wateja wetu watahamia kwenye laini za eSIM kulingana na faida zake kwenye matumizi. Ni Imani yetu kuwa wateja wetu na Watumiaji wa eSIM watafurahia ubunifu huu wa kidigitali. aliongeza Singano.
Katika hatua nyingine, Msanii wa kizazi kipya maarufu kama Diamond Platinum na ambaye pia ni balozi wa Kampuni ya Airtel ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwa ya kwanza kuleta kwenye teknolojia ya eSIM huku akiahidi kuendelea kupeperesha bendera vizuri kwa kutangaza bidhaa na huduma za Airtel.
“Ninayo furaha kuwa kwenye Kampuni hii ambayo inathamini sana bidhaa zenye bunifu na kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wake. Ukiwa na eSIM kutoka Airtel Tanzania sasa hakuna sababu ya kutembea na mzigo mkubwa wa simu kwani ili uwe umeunganishwa na laini zako, ukiwa na eSIM unaweza kutumia hadi laini tano kwenye simu moja”.
Ili kupata ESIM, tembelea kwenye duka lolote la Airtel nchini ambapo watoa huduma wetu atakuongoza kwenye mchakato mzima wa kubadilisha laini yako ya kawaida au na kupata laini mpya ya kidijitali ya eSIM.