NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
MFUKO wa Self Microfinance Fund umesema umejipanga kuondoa dhana ya kwamba watanzania hawakopesheki kwa kuwa sio walipaji wa madeni ya mikopo kwenye Taasisi za Kifedha.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Santiel Manongi leo Jumatano Oktoba 28,2025 kwenye Kikao Kazi baina ya Taasisi hiyo ,Ofisi ya Msajili Hazina na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam kueleza mafanikio waliyoyapata
Manongi amesema kuwa,Taasisi hiyo imejipanga kuondoa dhana hiyo kwa kujipima na kuhakikisha wakopaji wanarejesha mikopo kila wanapokopa kwa kuingia mikataba mipya au kuongezewa muda wa kulipa mikopo yao .
“Aliyekopa ni lazma arejeshe fedha alizikopa kwa kumuongezea muda hadi miaka miwili ya kulipa deni,kuingia mkataba mpya sambamba na kujua kwa nini mteja ameshindwa kulipia mkopo wake” amefafanua Manongi.
Akieleza mafanikio ya miaka mitatu ya Mfuko wa Self Microfinance,Manongi amesema imefanikiwa kuwa na matawi 12 yanayotoahuduma katika Kanda zote Tanzania nzima.
Aidha ameeleza kuwa Self inajivunia kutoa gawio hadi la Sh..Mil 490.9/- na faida ya Sh.Bilioni 3.19 baada ya Kodi.
Pamoja na mambo mengine,Self Microfinance Fund imefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 262,624 mwaka 2024-25 na mikopo kwa wakulima mbalimbali nchini.
Sambamba na hilo ,Manongi anajivunia mafanikio ya kuwa sehemu ya mradi kampuni ya Positive Cooker wa kutoa mikopo ya majiko ya nishati safi yanayotumia umeme mdogo na ukopeshaji wa Bajaji na Pikipiki na wajasiriamali wadogo.
Katika hatua nyingine Manongi ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mafanikio ya Mfuko wa Self Microfinance Fund.





