NA MWANDISHI WETU,SUMBAWANGA,RUKWA
WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, leo Jumanne Oktoba 13, 2026 amewasili Sumbawanga, mkoani hapa na kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru yanayotarajiwa kufanyika mkoani hapa kesho Jumatano Oktoba 14, 2026.
Mgeni Rasmi katika hafla ya kilele hicho anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi.











