NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WANAWAKE na wasichana wameshauriwa kuendelea kutumia vipimo sahihi katika kupima vitu mbalimbali katika biashara zao au vyakula vya nyumbani ili kuleta maendeleo ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa TUGHE Wanawake kutoka Wakala wa Vipimo (WMA) Nusura Chipatukila wakati akitoa salamu ya siku ya wanawake duniani itakayofanyika Machi 8, yenye kauli mbiu ‘Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe haki, usawa na Uwezeshaji’.
“Nawashauri wakinamama kuendelea kutumia vipimo sahihi na kuleta maendeleo ya nchi, wanawake wakiwa ni wadau wakubwa wa kutumia vipimo kwa kwenda kununua bidhaa mbalimbali au kupima vyakula vya nyumbani ni muhimu kutumia vipimo sahihi na pale unapokwenda na kukuta vipimo havipo sahihi toa taarifa WMA ili tuchukue hatua,” amesema