NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Novemba 03, 2024 amehani msiba wa Mzee John Tutuba ambaye ni baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba nyumbani kwa Gavana huyo Oysterbay jijini Dar es salaam
Mzee Tutuba alifariki Novemba 01, 2024 katika Hospitali ya Shifaa Pan African ya Kinondoni jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa.