NA MWANDISHI WETU, RUVUMA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya wa Tunduru mkoani hapa imewahukumu Viongozi wanne wa Chama cha Ushirika cha Majimaji Issa Rashid Makopi (Mwenyekiti),Mtuva Said Rashid(Meneja Msaidizi),Mfaume Zuberi Mambo (Meneja) na Halifa Saidi Chipangula (Meneja) kifungo cha miaka miwili jela na kulipa faini ya adhabu ya kulipa faini ya Sh. 1,500,000/- kwa kosa la kutoa hongo Sh.800,000/- George Alanus Njogolo kwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( Takukuru) Wilaya ya Tunduru ili asiendelee na uchunguzi dhidi yao.
Uchunguzi huo ulihusu ubadhirifu wa mbolea aina ya Salfa inayotolewa bure na Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (TAMCU LTD) kwa wakulima wa korosho waliopaswa kupewa na Viongozi hao kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na(2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [Sura ya 329 mapitio ya 2022]
Hukumu dhidi ya Viongozi wa hao ni katika shauri la Jinai Na. 26462/2024 ilitolewa Septemba 18, 2024 na Shughuli Mwampashe Hakimu Mkaazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya Tunduru akishirikiana na Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Mwinyi Yahaya.
Pamoja na adhabu hiyo, Sh.800,000/- imetaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hata hivyo washtakiwa wamelipa faini hiyo na wameanza kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.