NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma pamoja na viunga vyake wametakiwa kutembelea katika viwanja vya maonesho ya kilimo nanenane hususani katika banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa ajili kupata uelewa juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa zao.
Ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutatuliwa changamoto zao pamoja kupatiwa elimu sahihi pale ambapo watafika katika banda hilo kwa lengo la kujengewa uwezo na kupata huduma ya usajili wa bidhaa zao na kwa kuziongezea ubora bidhaa hizo.
Akizumgumza na Wananchi na Waandishi wa Habari Ofisa Kumbukumbu BRELA,Farid Hoza amesema mwananchi akifika katika banda hilo watapata uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa ambazo wanazizalisha na kuziongezea ubora kwa kiwango kinachokubalika.
“Tunawasaidia wanawasaidia wakulima, wafanyabishara kuweza kufanya maombi yao ya usajili.
” Katika haya maonesho tunafanya usajili wa papo kwa papo kitu ambacho sio rahisi na kama ulikuwa na changamoto ya muda mrefu haitatuliki ukija kwenye banda letu la Brela tunakusaidia Baraka, ” amesema na kuongeza
” Tunatoa elimu kitu ambacho unaweza usikipate ukiwa nyumbani lakini ukija hapa tunakupa elimu, ”
Pia amesema kwamba kutokana na umuhimu wa kujisajili wamekuwa wakitembea mikoani mbalimbali kutoa elimu ambapo hadi sasa wanufaika niwengi kwani wameshatembea takribani mikoa yote ya Tanzania pamoja na kuwafikia wakulima na wafanyabishara na bado wanaendelea kwani zoezi hilo ni endelevu.
Hadi sasa waneshasajili Kampuni zaidi ya 50 kwenye Maonesho hayo ya Nanenane.
“Wito wananchi kuudhuria katika maonesho ili kusajili biashara zao unaposajili unatambulika kisheria
Brela wapo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni ambapo wapo kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara, usajili wa kampuni,usajili wa alama za bishara na usajili wa Hataza na usajili wa leseni kundi A
Mmoja wa wateja wa BRELA,Yahaya Hassan amefika katika banda hilo kufuatilia taarifa za kampuni yake huku akikiri kuwa kapata huduma nzuri na kuhudumiwa kwa haraka.
“Huduma nzuri nimefurahi kwani nisingekuja hapa kwenye maonesho ingenilazimu kusubiri kwa muda wa siku tatu kwakuwa timu ya Brela iko hapa kila kitu inamalizwa hapa.
Nashauri wote wenye changamoto ya makampuni, au majina ya biashara nivyema kusongea kwenye banda la Brela ili wapate huduma kwa haraka”amesema.