NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo – Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni, jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, Dk. Jafo ameipongeza Benki Kuu kwa jitihada zake za kuelimisha wananchi kuhusu masuala muhimu katika sekta ya fedha na usimamizi wa uchumi nchini.