NA DANSON KAIJAGE,DODOMA
WATANZANIA wamehimizwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao badala ya kuwa na imani potofu ya kwenda kwa Waganga wa Kienyeji kwa imani za kurogwa wanapotetereka kiafya.
Ushauri huo umetolewa na Ofisa Programu (MKUTA) Mkoa wa Dodoma Rachel Jalibu,alipokuwa akizungumza na wananchi waliotembelea katika banda hilo katika viwanja vya maonesho ya kilimo nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Akizungumza na wananchi pamoja na Waandishi wa Habari Ofisa Programs huyo amesema kuwa wananchi wana kila sababu ya kupima afya zao na kupatiwa ushauri pale ambapo watabainika kuwa wamepatwa na magonjwa.
Hata hivyo amesema wagonjwa wote wanaogundulika kuwa wana ugonjwa wa kifua kikuu wanapatiwa matibabu bure pamoja na huduma zote za kimsingi.
Ameeleza kuwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu wanapopatiwa dawa za matibabu wakizitumia kwa usahihi wana uwezekano mkubwa wa kupona na kuendelea na shughuli zao kama kawaida wakiwa na afya njema.
“Napenda kutoa wito kwa watanzania wote kujenda utamaduni wa kupima afya zao na wanapopima afya wanakuwa nanuhakika wa afya na pale inapotokea kuwa na changamoto wanapatiwa matibabu kwa haraka.
“Kwa hapa Dodoma vituo vyote vina huduma ya kupima ugonjwa wa kifua kikuu na kutoa huduma zote za kimatibabu bure na ikitokea mgonjwa akahitajika kupima kwa kutumia mashine za mionzi atachangia kiasi kidogo ambacho ni Sh.10,000