NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
JUNI 28 mwaka huu Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 48 yalianza rasmi ambapo Shirika la Bima la Taifa NIC Insurance ni miongoni mwa Washiriki wa maonesho hayo ambayo yanafikia tamati Julai 13 mwaka huu.
Katika kipindi hiki cha Msimu wa Maonesho haya NIC Insurance imekuja na huduma tatu mpya amabzi zinadhihurisha kauli mbiu yao ya sisi ndio Bima.
Huduma hizo ni Bima ya Comesa,Majaliwa na Nisogeze.
Huduma hizi tatu mpya zinaendelea kutanua wigo wa huduma zake ambapo sasa huduma ya Bima ya COMESA inapatikana katika matawi yote yaliyopo kwenye mipaka yote yaTanzania.
Ifahamike kuwa COMESA ni Soko la Pamoja la nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, likijumuisha nchi wanachama 13 ambazo ni Tanzania, Burundi, DR Congo, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Sudan, Uganda,Zambia, na Zimbabwe.
Bima ya COMESA ni mahsusi kwa Watanzania wanaosafiri na vyombo vya moto kwenda nchi wanachama wa COMESA pasipo kuhitaji bima nyingine ya utatu ambayo ni ya lazima kisheria kwa vyombo vyote vya moto.
Akizungumza na juu ya Bima hiyo Ofisa Bima,Enid Zakayo anaiambia Demokrasia kuwa NIC Insurance ni wasimamizi wa utoaji huduma wa bima ya COMESA hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa fidia stahiki pindi mteja apatapo ajali na kusababisha uharibifu wowote wa mali au chombo cha moto kwa mtu wa tatu.
“Ili kupata bima hii,mteja anapaswa kutoa taarifa za safari yake, ni muda gani atakuwa nje ya nchi ili aweze kulipia gharama za bima yake kulingana na muda wa safari na matumizi ya chombo chake cha moto.
“Kupitia Bima hii mteja anaweza kukata kuanzia siku 10 hadi mwaka mmoja, ambapo mteja atalipia Sh.5000 ya kadi(COMESA yellow card) na Sh.8000 kwa kila kiti cha abiria ikiwa ni gharama ya matibabu kwa abiria au mtu wa tatu atakaye husika katika ajali hiyo” amefafanua Ofisa huyo wa NIC Insurance
Zakayo abasema Bima ya COMESA itamsaidia mteja kutumia chombo cha moto akiwa kwenye nchi tajwa bila wasiwasi wowote.
Aidha anaongeza kuwa Bima hiyo ni muhimu sana na ina manufaa makubwa hivyo Watanzania wanaosafiri kwenda nchi hizo kuchangamkia Bima hiyo.
Udhihirisho wa pili ni huduma ya Mikopo midogo midogo na ya muda mfupi iitwayo Nisogeze
Sababu za kuanzishwa kwa huduma hiyo ambayo ni ushirikiano wa NIC Insurance na Benki ya Taifa ya Biashara (TCB) ni kutatua changamoto za muda mfupi za kifedha zinazowakabili wateja wa Bima za maisha.
Akizungumza na kuhusu huduma hiyo ,Ofisa Bima wa NIC Upendo Shengena amesema kigezo kikuu cha kujiunga na Nisogeze ni kuwa na hati ya Bima ya Maisha kutoka NIC Insurance.
Ofisa huyo wa Bima anasema wakati ambao mteja anaweza kuanza kunufaika na huduma ya Nisogeze ni kuchangia ada kuanzia mwezi mmoja .
Akielezea Bima za Maisha zinazotoa faida ya Mkopo wa Nisogeze Shengena anasema ni Bima ya malengo ya miaka 20,Bima ya maisha iliyoboreshwa ya miaka 10 au 11,Bima ya Matumaini(Flex) ya miaka 9 ,Bima ya Majaliwa ya miaka mitano na Bima ya maisha ya elimu ya miaka mitano na kuendelea.
Pia Shengena anabainisha kuwa ili kupata huduma hiyo mteja anapaswa kujaza fomu ya kuomba kujiunga inayopatikana kwenye Ofisi za NIC ,kwenye tovuti pamoja na Matawi yote ya Benki ya TCB.
“Mteja akitaka kuomba mkopo wa Nisogeze atafungua simu yake ya kiganjani na kubonyeza 150*44 kisha atafuata maelekezo ambapo kiwango cha mkopo kitategemea na kiasi cha akiba kilichopo kwenye Bima ya maisha ya mteja” anafafanua Ofisa huyo wa Bima
Katika hatua nyingine,anasema muda wa kurejesha mkopo wa Nisogeze ni matakwa ya mteja ingawa ni kuanzia saa 24 hadi miezi sita ambapo akimaliza kulipa mkopo wake anaweza kuomba mkopo mwingine lakini akishindwa kulipa hataweza kupata mkopo mwingine ila mkopo wake utakuja kulipwa mwisho wa mkataba kulingana na akiba aliyojiwekea kupitia Bima yake ya maisha.
“Iwapo mteja atafariki akiba yake ya Bima ya Maisha haitaathirika kwa kuwa mkopo wake utafutwa na mafao ya Bima yatalipwa kwa mujibu wa utaratibu na sheria za mirathi.
” Na iwapo mteja atasitisha kuchangia Bima ya maisha hawezi kuendelea kupata mkopo wa Nisogeze kwa kuwa hatakuwa na akiba”anajinasibu zaidi.
Akielezea tofauti ya Nisogeze na huduma zingine zilizopo sokoni,Shengena anasema Nisogeze inatoa jawabu la haraka kwa changamoto ya kifedha kwa wateja wa Bima za maisha kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu kwa kutumia simu ya mkononi sambamba kuwaondolea Wateja usumbufu wa gharama zitokanazo na mikopo.
Udhihirisho wa tatu ni ujio wa
Bima ya Maisha ya Majaliwa inayotoa dhamana ya kifedha kwa mteja au wategemezi wa mteja endapo mteja huyo atakuwa amekubwa na janga la kifo.
Ofisa Bima kutoka NIC, Deogratius Mlumba anasema bima hiyo ni ya miaka mitano hadi 30 na kwamba inampatia fursa mteja kujiwekea akiba kidogokidogo kila mwezi na baadaye anapata akiba yake pamoja na faida inayopatikana.
Anasema endapo mteja atakumbwa na janga la kifo wategemezi wake watapatafaida na michango ambayo ilikuwa ikiwekwa na mteja hiyo katika bima hiyo ya maisha.
Mlumba anasema bima hiyo inamfaa mtu yeyote yule anayejiingizia kipata, mfanyabiashara au mfanyakazi kwani kima chake cha chini kabisa cha kuchangia ni kiasi cha Sh. 5000 huku cha juu ni kiasi chochote kile alichonacho mteja.
“Faida ya bima hii inatoa mafao ya Bima ya Maisha yanayozingatia thamani ya mfumko wa bei kwa kulipa zaidi kiasi alichochangia mteja, endapo mteja atapatwa na kifo familia yake itapata fidia ya asilimia 100 ya thamani ya bima,” anasema Mlumba
Aidha anasema bima hiyo ya Maisha ya Maajaliwa ina mafao moja ni mafao ya ukomo pili mafao ya kifo endapo mteja atapatwa muda wowote ndani ya mkataba.
Anasema katika mafao ya kifo ni fidia inayolipwa kwa wategemezi endapo mteja atafariki muda wowote baada ya kujiunga na Bima ya Maajaliwa.
Mlumba anabainisha mafao ya kumaliza mkataba ni mafao ambayo yatalipwa kwa mteja endapo atamaliza muda wake wa mkataba wa Bima ya Maisha Majaliwa.
Alisema mteja akishindwa kuendelea kuchangia Bima anaweza kufanya yafaatayo moja ni kupunguza thamani ya Bima ili aweze kuendelea kuchangia au anaweza akaacha kuchangia na kusubiri mpaka ukomo wa mkataba wake.