NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni, 2024, amepokea gawio la kiasi cha Sh. Bilioni Kumi na Nane Mia Tisa Sabini na Tatu, Millioni Mia Nane Hamsini na Tatu Elfu, Mia Tano Kumi na Nne na Senti Ishirini na Saba tu (18,973,853,514.27) kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ikiwa ni utekelezaji wa utoaji gawio kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Dk.Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA na Godfrey Nyaisa Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.