NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema serikali yake itadumisha ushirikiano na mahusiano na Benki ya CRDB.
Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Februari 20,2024 alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na ujumbe wake Ikulu Zanzibar
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya na Wakurugenzi mbalimbali wa Serikali kutoka Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.