NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua rasmi Mtaala wa Wakufunzi wa Elimu ya Fedha nje ya Mfumo Rasmi ambapo wananchi watapata elimu ya matumizi sahihi ya fedha ikiwemo akiba ili kuepuka mikopo umiza na kausha damu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BOT, Emanuel Tutuba alisema mtaala huo utakuwa na fursa nzuri ya kuona matokeo chanya katika shughuli mbalimbali kwenye upatikanaji wa mikopo, matumizi na hata urejeshaji kwa makundi ya wajasiriamali, wakulima, wavuvi na wengine.
Alisema wanafahamu changamoto ya mikopo chechefu inayotokana na kutokuwa elimu stahiki ya utaalamu wa fedha hivyo wanaendelee kushirikia wote ili kutoa elimu.
Tutuba alisema kuwa kila mmoja ana uwezo wa kushika fedha shida inakuja namna ya kuzitawala ambapo watu wanakuwa na matumizi mabaya hivyo mtaala huo utawawezesha kutoa elimu ili iwafikie wananchi.