DAR ES SALAAM, TANZANIA
Time ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu kucheza mashindano ya Mataifa Afrika (Afcon) baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi F.
Taifa Stars imejikatia tiketi baada ya kuifunga Niger leo Jumapili kwa goli 1-0 na kufikisha alama 7 ikifuatiwa na Uganda yenge alama 4 na Niger yenye alama 2.
Baada ya mchezo wa Stars na Niger kukamilika, ulianza mchezo wa Algeria na Uganda ambao ulimalizika kwa Uganda kulala kwa Magali 2-1.
Kama Uganda ingeshinda mchezo huo basi yenyewe ingesonga mbele na kuiacha taifa stars.
Hii ni mara ya tatu kwa timu ya Taifa ya Tanzania kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980 na mara ya pili ilikuwa mwaka 2019. Mashindano ya mwaka huu yatafanyika nchini Ivory Coast.
SOMA;