NA MWANDISHI WETU, IRINGA
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amesema, kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Iringa kutaleta faida kubwa kwenye kufungua utalii na kurahisisha mawasiliano na usafiri katika ukanda wa nyanda za juu kusini.
Katibu Mkuu ameyasema hayo leo alipotembelea mradi wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege Iringa ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara yake ya siku saba yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama na kukagua utelekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2023.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.