NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
BENKI ya NBC imetajwa kuwa miongoni mwa wadau wa maendeleo ikiwepo kudhamini mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umeitaja kwa kutangaza kazi zake.
Akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha Mkurugenzi wa watejea binafsi na wateja wadogo Elibariki Masuke amesema benki hiyo tangu imeanzishwa mwaka 1967 imekuwa mdau wa maendeleo kwa taifa ikiwepo kwenye sekta ya michezo.
Masuke amesema wameendelea kudhamini mkutano wa ALAT ambao huwajumuisha watumishi kutoka kila halmashauri na wilaya na kuomba sapoti yao kwani wamekuwa wakitoa mikopo na kusogeza huduma kwa wananchi kupitia njia ya kidijitali.
“Benki yetu ya NBC imekuwa mdau wa maendeleo toka mwaka 1967 tangu imeanzishwa hivyo wataendelea na adhima hiyo kwa kuleta maendeleo kila kona ya Tanzania ikiwepo kuboresha huduma zake kila wilaya”, amesema Masuke.
Masuke ameongeza kuwaBenki hiyo na ALAT wamekuwa wakishirikiana pamoja katika kuboresha utoaji wa mikopo kwa watumishi kwenye halmashauri 184 nchini.
Katika mkutano huoMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) unaofanyika katika Ukumbi wa Simba AICC jijini Arusha.