NA ANDREW CHALE, DAR ES SALAAM.
KAMPUNI ya Lodhia ambao ni wazalishaji wa bidhaa za ujenzi hapa nchini inayotengeneza bidhaa za chuma na Plastiki ipo mbioni kuongeza soko la ajira kwa kuanzisha kiwanda kipa cha uzalishaji mabati katika kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwenye Sera ya uwekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Lodhia, Sailesh Pandit katika maonesho ya bidhaa za viwandani yaliofanyika kwa siku mbili yakienda sambamba na mkutano wa bodi ya wakandarasi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es salaam tarehe 25-26,Mei mwaka huu.
Pandit amesema kuwa, Sera nzuri ya uwekezaji imeendelea kuwapa fursa ya kuwa mbioni kuja na kiwanda hicho cha mabati ambacho kitaanza kazi mwakani 2024.
“Tunaishukuru Serikali kwa namna inavyoonyesha nia katika miradi mkubwa inayojengwa kutumia bidhaa zetu za ndani.
Hivyo Lodhia katika kuongeza ajira nyingine ni kwa kuanzisha kiwanda cha uzalishaji wa mabati ambayo yatakuwa imara na ya kipekee.” amesema Pandit.
Aidha, Pandit ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuthaminina kutumia bidhaa za ndani ili kuleta tija kwa kuongeza ajira na kukuza uchumi.
Pia ameishukuru Serikali kwa namna inavyoonyesha nia katika miradi mikubwa inayojengwa kutumia bidhaa ikiwemo ya kiwanda hicho cha ndani.
Naye Mwenyekiti Msaidizi wa kampuni hiyo ya Lodhia, Mihiri Anand ameiomba Serikali kuharakisha mradi mkubwa wa bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo Rufiji Mkoa wa Pwani ili kusaidi kukabilina na changamoto ya umeme katika uzalishaji utakaosaidia kupunguza gharama katika matumizi ya nishati hiyo.
Ongezeko la viwanda mbalimbali hapa nchi utasaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa watanzania sanjari na kuongeza ujuzi ili kujikwamua na kuwa tegemezi.