NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema imezindua kampeni ya TUWAJIBIKE inayohamasisha wafanyabiashara kuwajibika kutoa risiti halali ya mashine za kielektroniki ( EFD) kila wauzapo bidhaa na wanunuzi kuhakikisha wanapewa risiti halali.
Mkurugenzi wa Elimu Kwa Mlipa Kodi kutoka ,TRA, Richard Kayombo amesema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumzia kuanza Kwa kampeni hivyo nchi nzima.
Amesema mwananchi anawajibika kudai barua inayomhalalishia mfanyabiashara kuuza bidhaa bila kutoa risiti za mashine za kielektroniki (EFD).
Imesema barua hiyo iwe imehalalishwa na TRA kwenda Kwa mfanyabiashara husika na itumike Kwa saa 48 pekee lakini wakati huohuo mfanyabiashara huyo aendele kutoa risiti za mkono.
Amesema mameneja wa mikoa nchi mzima watafiatilia utolewaji wa risiti halali na hatua zitachukuliwa kwa wanaokiuka ikiwemo adhabu na faini mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
.
Amesema kampeni imelenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibika kudai risiti halali ya EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu.
Amesema wananchi wanaponunua bidhaa wanastahili kudai risiti na kuhakikisha wanaikagua Ili kujiridhisha inakidgi vigezo vinavyotakiwa.
Amesema kampeni imelenga kufuatilia utoaji wa risiti halali za EFD nchi nzima pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofata sheria katika utoaji wa risiti halali za EFD zikiwemo
Kutoa risiti yenye mapungufu kama kuwa na kiwango cha chini kulingana na thamani ya halisi ya bidhaa au huduma, Kutumia risiti moja ya kushinikiza mizigo, Kufanya biashara ya kuuza risiti pasipokuwa na baishara yeyote.
“Risiti halali ya EFD inatakiwa kukidhi vigezo vikuu vinne ambavyo ni Jina la biashara, tarehe halisi ya mauzo, Kiasi halisi cha pesa kilichonunuliwa bidhaa au huduma Jina au TIN ya mnunuzi au vyote kwa pamoja,” amesema.
Amesema adhabu ya mfanyabiashara atakayebainika kutokutoa risiti halali ya EFD au kufanya udanganyifu atatozwa faini ya sh milioni tatu mpaka shmilioni 4.5 au kifungo cha kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Kayombo amesema kwa mnunuzi atakaebainika kufanya manunuzi bila ya kudai risiti halali ya EFD atatozwa faini ya shi 30,000 mpaka sh
milioni 1.5.
Aidha amesema zipo biashara sugu za kutuma vifurushi ambazo risiti hazitolewi ambalo ukaguzi utafanyika pamoja na eneo la burudani kwenye baa,hotel na migahawa ambalo kuna upungufu wa utoaji risiti.