NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Philip Mpango amemjulia hali Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk. Festo Dugange leo Aprili 29, 2023 wakati alipofika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa baada ya kupata ajali ya gari.
Taarifa ya Tamisemi iliyotolewa leo inasema kuwa Dk.Dugange alipata ajali usiku wa Aprili 26, 2023 wakati akiendesha gari yake binafsi Jijini Dodoma ambapo kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa.