NA MWANDISHI WETU, KATAVI
WAKAZI wa Mkoa wa Katavi wameondokana na adha ya kusafiri nje ya mkoa kufuata huduma za matibabu ya macho.
Akizungumza baada ya kuzindua jengo la huduma za matibabu ya macho lililofadhiliwa na Shirika la Ujerumani la TanZanEye kupitia kanisa la Katoliki jimbo la Mpanda, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesema kituo hicho kimekuja wakati sahihi na unaohitajika.
![](https://habarileo.co.tz/wp-content/uploads/2023/04/5d345f11-46a6-4eb0-973e-772a5d8cecf7-300x160.jpg)
RC Mrindoko amewataka wananchi wa huo na mikoa jirani kutumia kituo hicho kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kujua afya ya macho yao inavyoendelea ili kuweza kupata huduma stahiki mapema na kuhakikisha afya ya macho haitetereki.
Ameiagiza ofisi ya mganga mkuu wa mkoa pamoja na sekta ya afya kwa ujumla mkoani humo kuhakikisha kwamba wanatoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo ya macho inatolewa kwa ufanisi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk Jonathan Budenu amesema watu 192,000 sawa na asilimia moja ya wakazi wa mkoa huo wamebainika kuwa na matatizo mbalimbali ya macho katika mwaka 2022.
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi mwakilishi mkazi wa shirika la TanZanEye, Ryner Linuma, amesema hadi kukamilishwa kwa mradi huo pamoja na vifaa vyake vyote utakuwa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.090.
![](https://habarileo.co.tz/wp-content/uploads/2023/04/ef91caa8-4491-4594-89cb-9b3f4556c12e-2-300x165.jpg)
Linuma amesema Sh. milioni 658 ni ujenzi wa jengo na uboreshaji wa mazingira ya nje, na sh. milioni 332 ni manunuzi ya vifaa tiba na visivyo vifaa tiba, huku Askof wa Jimbo Katoliki Mpanda, Eusebius Nzingilwa, amewataka watoa huduma katika kituo hicho cha mtakatifu Alois, kuzingatia maadili ya utoaji huduma kwa jamii.
Mkurugenzi wa mradi huo wa macho, Dk Karsten Paust amesema huduma zitakazo tolewa katika hospitali hiyo ya macho haitowalenga wakatoliki pekee bali wananchi wote wa Mkoa wa Katavi.
![](https://habarileo.co.tz/wp-content/uploads/2023/04/216d324a-41e5-44bf-b862-0cc97930bb43-300x162.jpg)
Hata hivyo uzinduzi wa jengo hilo umeenda sambamba na zoezi la upandaji miti katika eneo