NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAGULIO ya simu yametoa ahueni kwa wananchi ambao wamenunua simu kwa kulipia kidogo kidogo kupitia programu maalum iliyowekwa na Samsung kwa kushirikiana na Tigo.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari inasema kuwa kupitia programu hiyo wateja wataweza kuchagua kati ya simu aina ya A04 na A04s na kulipa kuanzia Sh 1,000 kila siku kwa muda wa mwaka mmoja.
Taarifa hiyo inasema kuwa magulio hayo yameandaliwa na kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na Samsung kuanzia Aprili 17 jijini Dar es Salaam na Mwanza.
“Gulio hili pia litazinduliwa Kibo Complex-Tegeta Mei 4. Magulio hayo yatakamilika Mei 14, 2023 ili kuwapa wateja mwezi mzima wa kufanya manunuzi ya simu za Samsung na kufurahia zawadi zenye kusisimua na vufurushi, “imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema pamoja na kupata unafuu wa kulipia simu hizo, wateja pia watapata uzoefu wa simu mpya za Samsung Galaxy S23 (S23 Ultra; S23 Plus na S23) pamoja na toleo jipya la A series (A34 na A 54 5G)