NA MWANDISHI WETU, KILIMANJARO
MVUA zilizoanza kunyesha usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Aprili 3, 2023 katika maeneo mbalimbali mkoani hapa zimesababisha mafuriko na kukatika kwa mawasiliano katika barabara kuu ya Moshi-Arusha eneo la kwa Msomali Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amekiri kutokea kwa adha hiyo na amesema maji hayo ni mengi na kwa sasa hakuna magari yanayoweza kupita kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
“Ni kweli kwa sasa eneo la kwa Msomali halipitiki maji ni mengi kupita kiasi, magari yamesimama kwa muda na hayawezi kutoka upande wa Moshi kwenda Arusha na upande wa Arusha kwenda kuja Moshi,” amesema.