Manchester Utd wamnyatia Goncalo Ramos
MANCHESTER United wapo kwenye mawindo ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica na Ureno Goncalo Ramos (21) ambaye ana kipengele cha kuondoka kwenye klabu yake kama anayemtaka ataweka mezani Pauni Milioni 105.6m (Tsh. Bilioni 103.3)
Evan Ferguson aikacha Manchester United

Mshambulizi Evan Ferguson (18) ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland amepuuza uvumi wa kuhamia Manchester United akieleza kuwa yupo salama na mwenye furaha zaidi kwenye klabu yake ya sasa.
Manchester United yasaka mbadala wa David de Gea

Manchester United wapo kwenye mawindo ya kumsaka kipa makini na macho yao yametua kwa blinda mlango wa Brentford, Mhispania David Raya (27) ambaye atakuwa mbadala wa David de Gea (32), ambaye bado hajakubali kusaini mkataba mpya Old Trafford.
Chelsea yaweka dau kumnasa Victor Osimhen

Chelsea wameweka dau mezani kiasi cha Euro milioni 100 (Tsh. Bilioni 253) ili kumnunua mshambuliaji wa Nigeria anayekipiga Napoli, Victor Osimhen (24). Wakati huo huo, Chelsea wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Ufaransa, N’Golo Kante (31), kuhusu mkataba mpya wa miaka miwili.
Chelsea wasikitishwa na Thomas Tuchel

Arsenal yajitosa kwa Moises Caicedo

Arsenal imejitosa kutaka huduma ya kiungo wa kati wa Brighton na time ya taifa ya Ecuador, Moises Caicedo (21) msimu wa huu wa joto.
Alex Oxlade-Chamberlain azigonganisha klabu tatu EPL

Aston Villa, Newcastle na Brighton wanapigana vikumbo kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza, Alex Oxlade-Chamberlain (29) ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Sergio Busquets awatuninshia msuli Barcelona

Kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets (34) bado hajakubali mkataba mpya aliowekewa mezani na Barcelona na anafikiria kuachana na magwiji hao wa soka Hispania. Wakati huo huo Barcelona wamejiondoa katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Ureno na Wolves, Ruben Neves (26)
Chelsea, Arsenal jino kwa jino kwa Onana

Chelsea na Arsenal wanatoana jasho kwenye kiyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji, Amadou Onana (21) baada ya kung’aa kwenye klabu yake hiyo kenye makazi kenye uwanja wa Goodison Park.