NAIROBI, KENYA
MSAFARA wa kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja One nchini Kenya, Raila Odinga umerushiwa mabomu ya machozi na Polisi waliokuwa wanazuia maandamano jijini Nairobi.
Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, Machi 27, 2023 katika eneo la Kawangware jijini Nairobi kwenye siku ya pili ya maandamano ya wafuasi wa umoja huo.
Odinga akiambatana na naibu wake katika Muungano huo Martha Karua, kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka na kiongozi wa chama cha Roots, George Wajackoyah, ni miongoni mwa viongozi wa upinzani waliorushiwa mabomu ya machozi kwenye msafara wao.
Dakika chache baada ya kuanza maandamano hayo huku msafara wa kiongozi huyo wa upinzani ukipita njia za uchochoroni, maafisa wa polisi waliwarushia mabomu ya machozi waandamanaji waliokuwa wakibeba matawi ya miti, mabango, sufuria ,na baadhi ya vyakula wakionyehsa hali ngumu ya Maisha.
Jana, Mkuu wa jeshi la Polisi Kenya, Japhet Koome alisema maandamano hayo ni haramu.
SOMA ZAIDI: