NA MWANDISHI WETU, MISRI
TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeibuka kidedea kwa kuinyuka timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) kwa bao moja bila.
Mchezo huo uliopigwa leo Ijumaa, Machi 24, 2023 kwenye dimba la Mamlaka ya Suez nchini Misri ulikuwa ni wa kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika ya mwaka 2023 (AFCON2023) yatakayofanyika Januari na Februari 2024.
Goli pekee la Taifa Stars liliwekwa nyavuni na Simon Msuva kwenye dakika ya 71 ya mchezo akiunganisha krosi safi kutoka upande wa magaharibi mwa uwanja iliyonyunyizwa na mlin
zi Dickson Job.