Rashford atikisa kiberiti
Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford (25), amesema hatasaini mkataba mpya na klabu yake hadi wamiliki wapya wa klabu hiyo watakapotangazwa.
Real Madrid wamkomalia Haaland
Real Madrid wameanzisha tena makati wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City raia wa Norway, Erling Haaland (22) , kutoka Manchester City kwenye msimu hug wa joto.
Bayern Munich wamtimua kocht.
Bayern Munich wamemfuta Kazi kocha Julian Nagelsmann na nafasi yake inapigiwa chapuo na kocha wa zamani wa Chelsea raia wa Ujerumani, Thomas Tuchel.
Tottenham Hotspurs njia panda
Tottenham inafikiria kumpa kazi kocha Nagelsmann kama mbadala wa Muitaliano Antonio Conte ambaye anaweza kutimuliwa muda wowote..
Chelsea, Manchester City, Newcastle United waingia vitani
Chelsea, Manchester City na Newcastle United Wako kwenye vita kali ya kuisaka saini ya winga wa Juventus, raia wa Uingereza, Samuel Iling-Junior (19).
Ilias Akhomach azichanganya Arsenal, Leeds Utd, AC Milan na Sevilla
Mchezaji wa Kimataifa wa timu ya chini ya miaka 19 ya Barcelona na Uhispania, Ilias Akhomach (18), anavinyima usingizi vilabu vya Arsenal, Leeds, AC Milan na Sevilla ambavyo vinatoana jasho la kutaka saini yake.
Luka Vuskovic kwenye rada za Manchester City na PSG
Mpango wa Manchester City wa kumsajili beki wa kati wa klabu ya Hajduk Split, Luka Vuskovic unawekewa kauzibe na klabu ya Paris St-Germain ambayo nayo inataka kumnunua Mkroatia huyo mwenye umri wa miaka 16.
Giovani awaniwa na Everton na Newcastle Utd
Everton wamejiunga na Newcastle katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Brazil Giovani (19), anayechezea timu ya Palmeiras ya Brazil.
Safari ya Messi kurudi Barca yanukia
Uvumi wa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi (35), kuondoka Paris St-Germain na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Barcelona unaongezeka.
Barca hatihati kucheza michuano ya Uefa mwakani
Barcelona huenda ikafungiwa kucheza soka la Ulaya kama Uefa itaikuta na hatia kwenye uchunguzi walioanza kuufanya kuhusu malipo yaliyotolewa kwa aliyekuwa makamu wa rais wa kamati ya waamuzi ya Uhispania.
Lindelof kuamua Lusaka ama kunyoa
Beki wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof (28), atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake kwenye klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu huu.
Glazer wawatia hofu wanaotaka kuinunua Man Utd
Wasiwasi unaongezeka miongoni mwa watu wanaotaka kuinunua Manchester United kwamba familia ya Glazer inaweza kuacha mango wa kuiuza klabu hiyo.