Liverpool kutomuongezea mkataba Keita
LONDON, UINGEREZA
UONGOZI wa kikosi cha Liverpool,nchini Uingereza kimeweka wazi kuwa uenda msimu ujao katika dirisha la usajili halitamuongezea mkataba mwingine kiungo wao wa kati Naby Keita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Guinea alijiunga na Liverpool Agosti 2017 akitokea katika klabu ya RBL ya nchini Ujerumani na licha ya kukabiliwa na majeraha mara kadhaa tayari amefanikiwa kuisaidia timu kubeba vikombe sita ukiwemo ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo.
Mwanandinga huyo miongoni mwa klabu zilizoanza kumkuza kisoka akiwa na miaka nane nchini kwao ni Horora AC, iliyokubali kipigo cha mabao 7-0 dhidi ya Simba ya Tanzania katika dimba la Mkapa Dar es Salaam.
Newcastle yamuwania winga wa Bayern Leverkusen
MUNICH, UJERUMANI
NEWCASTLE United wako katika mipango ya kutaka kumnunua winga wa Bayer Leverkusen Mfaransa Moussa Diaby(23) na beki wa kushoto wa Uholanzi Mitchel Bakker, 22.
Winga huo awali habari zilidai kwamba kwamba alikuwa akiwaniwa na vinara wa ligi kuu ya Uingereza Arsenal na mazungumzo yalikuwa yakiendelea kwa washika mitutu hao.
Hivyo inawezeka katika klabu hizo mojawapo inaweze ikafanikiwa kumnyakua kulingana na ofa itakayokubaliwa na klabu yake ya Bayern Leverkusen inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujeruman Bundesliga. Ujerumani.
Chelsea kujenga uwanja mpya
LONDON, UINGEREZA
KLABU ya soka ya Chelsea, nchini Uingereza inajipanga kuujenga uwanja wao wa Stamford Bridge kwa lengo la kuhakikisha unakuwa na ubora wa hali ya juu kimataifa.
Licha ya kwamba bado hajaeleza kuwa baada ya kuujenga upya utakuwa na uwezo wa kuingiza watu wangapi ingawa inakadilliwa kugharimu Euro Bil.2 hadi kukamilika kwake.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba wakati wa kipindi cha ujenzi wa uwanja huo, kikosi cha Chelsea kitakuwa kikitumia viwanja vingine vikiwamo vya Craven Cottage Twickenham na Wembly katika kipindi cha miaka minne.
(Mail)
Ten Hag kuongezewa makataba Man U
MANCHESTER, UINGEREZA
WAKATI Klabu ya Manchester United ikiwa mbioni kuuzwa kutokana na mazungumzo yanayoendelea kufanyika kwa sasa, wanatarajia kutomuongezea mkataba mwingine Meneja wa kikosi hicho Erik ten Hag
Mkataba ambao anaotarajia kuongezewa bosi huyo ni wa miaka mitatu jambo linalodhihirisha wameridhika na huduma yake tangu ajiunge na kikosi hicho cha Masheteni Wekundu.
Erik Hag