NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO Tanzania, imetambulisha rasmi toleo jipya la muendelezo wa Series ya SPARK ambayo ni TECNO SPARK 10 PRO.
Mkufunzi wa simu za TECNO Tanzania, Shakira Mkima wakati akitambulisha simu hiyo alisema TECNO SPARK 10 PRO ni simu ya kisasa na yenye gharama nafuu na sifa yake kubwa ikielekezwa kwenye uhodari wa MP32 za selfie kamera na MP50 za kamera ya nyuma, ambazo zinang’arisha picha na kuzifanya kuwa nau bora wa hali ya juu.

Sifa nyengine ambazo zinaifanya simu hii kuwa ya kipekee na yenye kuvutia ni wepesi wa bei ukilinganisha na unachokipata. Pamoja ya kuwa na kamera mahiri vilevile TECNO SPARK 10 PRO ina umbo la kupendeza lenye skrini ya inch 6.78 FHD, RAM ya GB8 inaongezeka hadi GB16, ROM ya GB256, toleo jipya la Android 13, processor G88 pamoja na warranty ya miezi 13”, alisema Shakira Mkima.
Katika kuikaribisha simu hii sokoni, TECNO Tanzania imeshirikiana kwa ukaribu na Kampuni ya Mawasiliano Tigo Tanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja wa Vifaa Tigo, Imeld Edward, amesema; “Uhusiano wa kuaminika tulionao na Kampuni ya simu TECNO una mchango mkubwa katika kuwapa wateja wetu vifaa bora zaidi. TECNO SPARK 10 PRO itafungua uwezo kwa wateja wengi zaidi kupata huduma zetu kupitia mtandao wetu wa 4G lengo letu ni moja kukuza maisha ya kidijitali nchini Tanzania na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma hivyo basi tunatoa ofa ya GB78 za intaneti bure kwa wateja wa TECNO SPARK 10 PRO”.

TECNO SPARK 10 PRO inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.