NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Dk Mehment Gulluoglu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na Uturuki na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili